1 Chronicles 2:1-6

Wana Wa Israeli


1 aHawa ndio waliokuwa wana wa Israeli:
Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni,
2Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.

Yuda

Hadi Wana Wa Hesroni


3 bWana wa Yuda walikuwa:
Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua.
4 cTamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.


5 dWana wa Peresi walikuwa:
Hesroni na Hamuli.

6 eWana wa Zera walikuwa:
Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.
Copyright information for SwhKC